Friday, May 24, 2013

Msaada wadau, Muarobaini wa Ujangili huu ni nini?

Kwa kweli kila ndugu zangu ninapotazama picha hii natamani kuwepo mjadala wa kitaifa juu ya hatma ya rasilimali hii ya wanyamapori hususani Tembo, maana kuna kila dalili kuwa kama hali itaendelea hivi sio muda mrefu Tembo watapukutika kama walivyopukutika Faru.

Hizi ni pembe za ndovu zilizokamatwa huko nchini China baada ya kubambwa na vyombo vya usalama vya China.
Tembo wakiwa na furaha lakini hizo pembe walizonazo ndizo zinazowaponza.

Haya wadau mnasemaje? Tujadili kwa busara na kwa faida ya Tanzania.