Monday, October 6, 2014

KUMRADHI SANAAAAAA

Kwenu wadau,
Kwa niaba ya timu yangu, nawaombeni radhi sana kwa ukimya uliodumu kwa muda mrefu. Kuna sababu za Msingi zilizosababisha haya yote. Lakini kubwa ni Mkakati mkubwa unaoandaliwa na Msigwa Blog katika kuhabarisha kwa uhakika, upana na undani. Naomba tuendelee kuvuta subira

Gerson Msigwa
DG Msigwablog

Tuesday, May 6, 2014

Wadau tuongeze juhudi kuinadi Tanzania



Ujumbe
Kwa takribani siku tatu nimekua safarini kikazi Pemba na Unguja na kisha Dar es salaam. 
Nadhani wadau bado tuna kazi ya kufanya kuzinadi fursa zilizopo katika maeneo yetu kimkakati. Kwa mfano fukwe zetu bado zinatumia kwa Uchuuzi wa Samaki, Kampuni ya Azam Marine sasa imetatua moja ya kero kubwa zilizokua zikikabili mawasiliano kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar nina maana kero ya Usafiri lakini bado hakuna joto la ushirikiano wa kimanufaa linaloonekana kwa kiasi cha kutosha kwa kutumia fursa hii mfano Ukuzaji Utalii wa Ndani na nje kati ya maeneo haya mawili, Hotel na mengine.

Nimejifunza kuwa Zanzibar bado inahitaji kutangazwa zaidi ya ilivyo sasa, Utamaduni wake, rasilimali zake hasa mazao ya marashi, Utamaduni wake nakadharika. Nimejifunza kuwa wawekezaji katika sekta ya Hotel Zanzibar wanapaswa kufanya zaidi ya ilivyo sasa ili pawe mahali pakukimbiliwa na hata watu wakipato cha Chini badala ya kuwategemea wageni pekee.

Nimejifunza kuwa sisi waandishi wa habari kwa kutumia rungu letu la Utangazaji na uchapishaji tuna kazi kubwa ya kuamsha, kujenga na kuimarisha Utalii wa ndani. tuwajenge watanzania kuwa Mtalii si lazima awe mgeni kutoka nje ya nchi. tunaweza kufanya hili.

Na kwa kuwa wakati huu Tanzania imefunikwa na joto la kuandika Katiba Mpya huku ajenda ya Muungano wa namna gani ikiwa imefunika kazi nzima ya Kuandika Katiba tuna kazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania juu ya safari hii ili imalizike kwa usalama. Safari hii iepuka mambo yatakayovuruga maziwa na asali waliyonayo watanzania wa bara na visiwani hata kama wengi wanaona haijawanufaisha wananchi. tuwawezeshe watanzania kupima hoja zinzotolewa ni kwa namna gani fursa hizi zitaathirika ama kupiga hatua.

Muhimu zaidi tufanye kazi hii tukiwa na mawazo huru na kutanguliza maslai ya Taifa Mbele. Najua hapa kuna chngamoto kubwa lakini Mungu aongoze

Gerson

Baada ya Kimya Kirefu

Kutoka kwangu,
Nikiri kwamba nimekua kimya kwa muda mrefu pasi kuweka kitu kipya kwenye Blog
Ahaa kama mnavyojua kubanwa na mengi ndio sababu. Hata hivyo tupo pamoja na tuendelee kuwa pamoja


Thursday, March 6, 2014

Msaada wadau kutambua majina ya wachezaji hawa wa Majimaji FC enzi hizo za Dr Gama

 

Mdau Mpenda Mvula Kanijaalia picha hii ya timu ya Majimaji ya Songea Enzi hizo za Bambo Gama (Dr Laurence Gama) lakini kanipa mtihani kutafuta majina ya kila mchezaji hapo. Msaada wadau.
 
Huyu ni Mzee Abdalah Ally, Mmoja wa waasisi wa timu ya Majimaji. Yeye na wenzake akina Mbegambega walikua na timu zao za soka zilizokua na nguvu Songea, alipokuja Dr Gama akawashawishi wavunje timu zao na kuunda timu ya Majimaji na wao wakawa viongozi. Kuna
habari kuwa Mzee huyu alikua mpenzi Mkubwa wa Majimaji FC kiasi kwamba miaka ya 80 Majimaji ilipofungwa na Yanga alipatwa na Upofu, Namtafuta mwanae Hamis Abdalah Ally athibitishe habari hizi. Mzee huyu ametangulia mbele za Haki Machi 02, 2014
siku ambayo Majimaji ilicheza dhidi ya Lipuli ya Iringa na Lipuli ilichapwa 2-0.